Habari

Breaking News:Waziri wa Muungano na Mazingira January Makamba adhibitisha kupatikana kwa MoDewij

MoDewij apatikana

Waziri wa Muungano na Mazingira January Makamba amerhibitisha kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa amepatikana mfanyabiashara mkubwa Mohamed Dewij na tayari ameonana nae na kuongea nae.

Makamba amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kusema hivyo.

Ikumbukwe kuwa MoDewij alipotea wiki moja iliyopita kwa kutekwa na watu wasiojulikana katika hoteli ya kifahari ya Clollesium Masaki jiji Dar es Salaam wakati anaenda hapo kwa mazoezi alfajiri ya Saa kumi na moja.

Taarifa hii inatokea baada ya jana IGP Kamanda Sirro kuongea na Waandishi wa habari na kuonyesha gari lililomteka kuwa sio la nchi hii bali ni la nchi jirani na kusisitiza kuwa uchunguzi bado unaendelea.

kwa habari zaidi kuhusu Mo endelea kufuatilia Bongo five kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii kujua zaidi.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents