Habari

Wazungu wampa ulaji

Wazungu wampa ulaji
Baada ya kutulia kwa muda mrefu bila kujihusisha na ishu yoyote ya
ukorofi kama alivyokuwa akifanya siku za nyuma, msanii Godfrey Tumaini
a.k.a Ze Dudu, ameibuka na kutamka kwamba cheo cha umeneja alichopewa
kwenye Kampuni ya Art in Tanzania kimemfanya awe na nidhamu ya kutosha

Dudu aliyasema hayo usiku wa kuamkia Juni 13, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa TTC Chang’ombe, Dar es Salaam ambapo kampuni yake ilikuwa imedhamini kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss Chang’ombe 2009 kilichofanyika katika ukumbi huo.

“Kutokana na nafasi niliyonayo kwenye kampuni hiyo, nitawashangaza sana mabosi wangu ambao wengi ni watasha kama nitafanya ishu za ukorofi ambayo ni mambo ya kizamani,” alisema Dudu.

Aidha, msanii huyo alisema kwamba, siku hizi hata kwenye kumbi za burudani amepunguza kwenda labda kama atakuwa amealikwa kwasababu ya shoo, siyo kuibuka bila mpango wowote kama ilivyokuwa zamani.

Ze Dudu ambaye ametamba kuvuta mkwanja mrefu kwenye kampuni hiyo, amesema kuwa staili yake ya kufanya muziki hivi sasa ni kutoa ngoma moja moja tu, hana mpango wa kugonga albamu kwakuwa singo inapokuwa bomba shoo utakazoalikwa zinalipa kuliko kuhangaika na maandalizi ya albamu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents