Burudani

WCB kuna mipaka yake – Rich Mavoko

Msanii wa Bongo Fleva ambaye yupo chini ya usimamizi wa lebo ya WCB, Rich Mavoko amesema si kweli kwamba yeye ana sauti kuzidi wasanii wengine ndani ya lebo hiyo kwani kuna mipaka ambayo kila mmoja anapaswa kuiheshimu.

Mavoko amesema wasanii wa WCB wanaishi kama watu wanaoishi na wazazi wao, hivyo linapokuja suala la kuchukua maamuzi au kutaka jambo fulani ambalo linahusisha uongozi ni lazima kufuata utaratibu.

“Mtu kama Tale, Sallam na Mkubwa Fella, useme tu kitu fulani na uamue wewe, huo ni uongo. Ni wakubwa kwangu, so hata kama tunaongea kuna mipaka lazima niwe naheshimu, ukisema sauti yangu ndio isikilizwe tu kwa desturi yetu na mila utakuwa unakosea,” Rich Mavoko amekiambia kipindi cha Twenzetu cha Times FM.

“Lazima uongee katika njia nzuri na wakuelewe, si semi nikiongea ndio litakuwa limepita kwa sababu mwisho wa siku umempa mtu nafasi ya kukusimamia maana yake umemuamini, pia anajua anachokifanya. Kwa hiyo unaleta mawazo nimeona hiki na hiki nataka nifanye, wao wanakaa na wanajadili kama kipo sawa mnafanya,” ameongeza.

Rich Mavoko ambaye alikuwa ameongozana na Rapper Stereo katika kutambulisha wimbo wao mpya ‘Mpe Habari, ameongeza kuwa WCB ni familia ya mwanamuziki yeyote wa Bongo Fleva ambaye anajitafutia maisha, anajituma na ana uwezo wa kazi wao wanampa nafasi.

Diamond na Stereo

Kwa upande wake Stereo alipoulizwa namna ilivyokuwa hadi kufikia hatua ya kufanya kazi na Rich Mavoko na kama kuna mpango wa kujiunga na lebo hiyo, alijibu “kimsingi WCB ni familia, hata sifikirii (kujiunga), yaani naona nimo tu, naona kama na mimi ni sehemu ya WCB,” amesema Stereo.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents