Habari

Weekend Recap: Zanzibar International Film Festival in Pictures

Bongo5.com ilitinga visiwani Zanzibar kuona ni yapi yaliyojiri katika tamasha la filamu la ZIFF.

Pamoja na onyeshwaji wa filamu mbalimbali za ndani na nje ya nchi, pia mlizinduliwa channel mpya na kampuni ya Zuku TV,iitwayo Zuku swahili, ambao Zuku walikua kati ya wadhamini wakuu wa Ziff.Tukio liliandaliwa rasmi sambamba na mdahalo wa kuangalia namna Zuku kwa kushirikiana na wadau wa Ziff kutoka sehemu mbali mbali za dunia wanaweza kuongeza mkazo katika kuchochea ari ya maudhui ya uzalendo ki Afrika kwa waigizaji, waandaaji na watengenezaji wa filamu barani Afrika.

Mdahalo huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Ziff 2012 bwana Thabit Kombo pamoja nae Meneja mtendaji wa Kampuni mama ya Zuku Wanainchi Group bibie Hennelie Bekker pamoja na wajumbe waalikwa kama Prof Issa Shivji (Tanzania), Prof Maggie Kigozi( Uganda), Medea Brown,(USA), Jackson Peter (Nigeria), amelie Thogersen (Denmark) na wengineo wengi kutoka Malawi, Afrika Kusini na Scotland.

Tukio la pili lilikuwa kuonyeshwa kwa filamu pamoja na burudani ya muziki iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa ya msanii jose Chameleone kutoka Uganda ambaye naye hakuwaangusha wapenzi wake baada ya kuwapa burudani kali ya nyimbo zake zaidi ya 8, ikiwemo Dorotia, Jamila, Valu Valu, Fitina, Kipepeo, Mama Roda na nyinginezo nyingi.

Angalia zaidi kwenye picha

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents