Burudani

Wema akwama kujiunga na CHADEMA, Sumaye aeleza sababu (Video)

Jumanne hii malkia wa filamu nchini, Wema Sepetu ameshindwa kujiunga rasmi na Chama cha Chadema na kukabidhiwa kadi ya uanachama kutokana na ratiba ya shunguli hiyo kuingiliana na ratiba ya Mahakama.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Fredrick Sumaye amesema muigizaji huyo alikuwa aende ofisini hapo kwaajili ya kuchukua kadi ya chama hicho na kujiunga rasmi.

Wema amepandishwa Mahakani leo saa nne asubuhi na kuambiwa atapandishwa tena leo jioni saa sita jioni hali iliyosababisha ratiba ya mkutano wake na waandishi kughailishwa.

Muigizaji huyo anatuhumiwa kukutwa na msokoto mmoja wa bangi nyumbani kwake baada ya kufanyiwa upekuzi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents