Burudani

Wema na Penny wote walikuwa rafiki zangu – Esma Platnumz

Dada wa Diamond Platnumz, Esma Platnumz amesema waliokuwa mawifi zake, Wema Sepetu na Penny hajawahi kugombana nao na hadi sasa ni marafiki.

Akizungumza na Times FM, Esma amesema licha ya warembo hao kuachana na kaka yake bado wapo sawa na kama kuna tofauti ni za kawaida.

“Kati ya Wema na Penny wote walikuwa rafiki zangu na tunaongea kama kawaida tukionana, tunacheka, tunamisiana, wote nipo nao sawa,” amesema Esma na kuongeza.

“Mawifi sisi kupewa lawama ni kawaida, tumeshazoea, ukiwa na wifi ni lazima utagombana nae hicho kitu hakizuiliki lakini sijawahi kugombana na mtu yeyote ila kwa kupishana mkiwa ndani ni kawaida,” amesistiza.

Katika hatua nyingine Esma amekanusha uvumi kuwa mrembo Hamisa Mobetto ni wifi yake na kusema wao ni marafiki wa kawaida na yanayoendelea ni maneno ya instagram.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents