Wema Sepetu aanza kuimba Bongo Fleva

Imebainika kuwa msanii wa Filamu Bongo, Wema Sepetu ameamua kuingia kwenye muzuki wa Bongo Fleva.

Prodyuza kutoka MJ Records, Daxo Chali ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa Wema Sepetu ameshiriksha katika wimbo wa Haitham ambao unatoka kesho, na kubainisha kuwa Wema ni muimbaji mzuri.

Daxo ameeleza kuwa awali alitaka wimbo huo afanye mwenyewe Haitham na ulipokamilika aliona kuna haja ya mtu mwingine kuwepo katika ngoma hiyo ingawa alisita kutokana Haitham wimbo wake wa kwanza alimshirikisha Mwana FA hivyo watu wataona anabebwa lakini alipokaa na kuweza aliona Wema anafaa ndipo wakamtafuta.

“Kuna siku kweli akaja, so tukamuingiza studio tukamuonyesha mashairi aingize wala hakusumbua, kwanza Wema anajua kuimba sema watu wengi hawajui ilo suala ila kitu kilichokuwa kinamsumbua sana ni zile melodi kwa sababu ile ngoma ni ya kiswahili lakini imeimbwa kama kifaransa, so ndio kitu kilichokuwa kinamsumbua sana ni kutamka yale maneno  lakini kwenye kukaa kwenye key yupo vizuri sana,” amesema Daxo.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW