Burudani

Wema Sepetu adai hana uwezo wa kuzaa, post yake yawaliza wengi!

Wema Sepetu ana huzuni moyoni. Amepata vyote lakini si mtoto na mbaya zaidi hana uwezo wa kumpata, kwa mujibu wa maelezo yake kwenye Instagram.

wema

Wema aliamua kuandika post ndefu kwenye Instagram kuelezea jambo hilo baada ya post ya mwanzo aliyokuwa akimpongeza Hamisa Mobeto kwa kupata mtoto kuambulia maneno ya kashfa kutoka kwa baadhi ya followers wake wasio wastaarabu.

“Ningekuwa na uwezo wa kuzaa ningekuwa nimezaa muda mrefu sana… But sina… Na siwezi kumkufuru mwenyezi mungu…. Au mngependa niwe nawaambia jinsi ninavyo hangaika usiku na mchana kupata mtoto wangu mwenyewe… Is dat wat u want…? kila ntakachofanya kwa ajili ya tumbo langu basi nitangaze… Au mnadhani siumii mnavyosema kuhusu maswala ya mtoto:(:(:(… Kumbukeni na mimi pia ni binaadam… Nina moyo kama nyie… Au mnadhani napenda kuona wenzangu wana watoto au wana ujauzito alafu mimi sina hata wa kusingiziwa… Mnaona nafurahia sio…. Hivi mna nini jamani,” ameandika.

“Yaani mtu unaweza weka post kwa nia nzuri then people jus come from nowea wanaanza kukuandikia maneno ya kukuumiza kabisa nafsi hadi mtu unakaa unajiuliza umemkosea nini mwenyezi Mungu… Kwani kuna niliemkosea yoyote mpaka muanze tu kunikashif na kunitolea maneno mazito namna hio… Kisa mtoto… Mnadhani naipenda hii hali… Hata mimi natamani kuitwa mama na hakuna kinachoniuma kama hicho…. So mnadhani sijui kama umri unaenda na maisha yenyewe sikuhizi mafupi anytime we die… Mnafikiria nisingependa kuacha hata ka copy kangu siku ndo Mungu anasema ananichukua… Hata mimi natamani ningekuwa napiga picha niko na mwanangu… I want dat with all my life but I cant…. Sitokaa nimkufuru Mungu wangu hata siku moja maana sijui ni kitu gani kaniandikia… But just dont rub it in… It hurts… And im jus a human being like each and everyone of u.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents