Diamond PlatnumzWema Sepetu

Wema Sepetu aeleza kwanini hampendi tena Diamond na kwanini Zari hamtishi kwenye fashion

Wema Sepetu hampendi tena Diamond Platnumz na anasema kila anapoukumbua uhusiano wao, anakumbuka mambo mabaya zaidi kuliko mazuri.

wpid-wema-akiwa-pembeni-kumsupport-diamond1.jpg

“Hapana simpendi [Diamond], yalishaisha hayo, nilishampendega, niliwahi kumpenda sana, lakini hamna tena, yaani hata sishtuki,” Wema alikiambia kipindi kifupi cha Kabali cha EFM.

“Nikimkumbuka Diamond most of the things ambavyo ninavikumbuka sio vitu vizuri na ndio maana hata sasa hivi imekuwa hivyo. Vizuri vilikuwepo lakini mtu anaweza akafanya vizuri akaja kufanya kimoja tu kibaya na akaharibu vyote tisa,” aliongeza.

Katika hatua nyingine Wema alisema Zari the Bosslady hamtishi katika sekta ya fashion.

“[Zari] hanitishi kwasababu yeye ana taste yake, mimi nina taste yangu, yeye ni Zari mimi ni Wema,” amesema muigizaji huyo. “I got my own, I like to play along with anything and she got her own.”

Msikilize zaidi hapo chini.

Related Articles

Back to top button