Burudani

Wema Sepetu alivyotimua mbio mahakamani baada ya kuachiwa kwa dhamana (Video)

Wema Sepetu(30) ameonywa kutokiuka masharti ya dhamana, vinginevyo Mahakama itamfutia dhamana. Wema alikuwa rumande siku 7 hadi leo kutokana na kushindwa kufika Mahakamani bila taarifa

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatayu, Juni 24, 2019 na Hakimu Mwandamizi wa mahakama hiyo, Maira Kasonde wakati akitoa uamuzi kuhusiana na mshtakiwa kukiuka masharti ya dhamana.

Juni 17, 2019 Mahakama hiyo iliamuru mshtakiwa huyo kupelekwa rumande hadi leo Jumatatu, ili iweze kutoa uamuzi baada ya mshtakiwa huyo kujisalimisha mahakamani hapo.

Wema alijisalimisha mahakamani hapo Juni 17, 2019 baada ya Mahakama hiyo kutoa hati ya kumkamata mshtakiwa huyo kutokana na kushindwa kufika mahakamani bila kutoa taarifa.

Mahakama ya Kisutu, ilitoa hati ya kumkamata Wema, Juni 11, 2019 baada ya mshtakiwa huyo kuruka dhamana.

“Mahakama inatoa onyo la mwisho kwa mshtakiwa, ikitokea mshtakiwa huyu amevuja sheria kwa kutokufika mahakamani bila taarifa, Mahakama hii haitasita kumfutia dhamana.”

“Hivyo Mahakama imekurudishia dhamana yako na utakuwa nje kwa dhamana,” amesema Hakimu Kasonde wakati akisoma uamuzi wake dhidi ya mshtakiwa huyo.

Wema ambaye alishawahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2006, anakabiliwa na shtaka moja la kuchapisha video ya ngono na kusambaza katika mtandaoni wa Istagramu kinyume cha sheria.

Hakimu Maira ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 4, 2019 itakapoanza kusikilizwa ushahidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents