Burudani

Wema Sepetu amtambulisha mume wake mtarajiwa

Aweka mambo hadharani

Msanii wa Bongo Movie na aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 2006 Wema Sepetu ameamua kumtambulisha mume wake mtarajiwa kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Wema ameposti picha hiyo na mwanaume mmoja ambaye hakuweza kutambulika kwa haraka ingawa sura yake inaonekana,picha hiyo inaonekana kabisa Wema na mwanaume huyo wako kitandani wamelala ingawa mpiga picha ni Wema mwenyewe akipiga Selfie.

Ifahamike kwamba mrembo Wema amekaa muda mrefu bila watu kumtambua mwanaume wake kwani alishazoea kuwapost wanaume anaokuwa nao kwenye mahusiano,kipindi cha hapa katikati watu walihisi mrembo huyo yupo kwenye mahusiano na muigizaji kutoka nchini Ghana ambaye amefanya nae Movie waliyoitambulisha mwezi wa tisa ambayo inajulikana kwa jina la D.A.D, na maswali hayo aliulizwa kwenye mahojiano yake mbalimbali na vyombo tofauti vya habari ila wema alikataa lakini leo ameweza kumuweka hadharani mwanaume wake ambaye yeye anamuita “My future husband”.

Wema Sepetu amefanikiwa kuwa kwenye mahusiano tofauti tofauti na wanaume wengi hasa mastaa wengi wao wakitoka hapa Tanzania lakini hakuweza kudumu nao licha ya wengi kuonekana kama walikuwa na mahusiano ya kweli na watu walihisi watadumu lakini mwisho wa siku waliachana.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents