AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Wema Sepetu apata kigugumizi kuuzungumzia ugonjwa uliokuwa unamsumbua

Malkia wa filamu, Wema Sepetu Jumatatu hii alipata nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari muda mchache baada ya hukumu ya kesi yake ya kutumia dawa za kulevya kupigwa kalenda hadi Ijumaa hii.

Moja kati ya vitu ambavyo alivizungumza mrembo ni pamoja na kipindi kigumu alichopitia wakati anaumwa.

“Ni kweli hapa katikati nilikuwa anaumwa lakani namshukuru Mungu nimepona,” Wema aliimbia Bongo5. “Siwezi kuzungumzia nilikuwa naumwa nini hiyo ni privacy yangu, sasa kama video mliiona ndio ni kweli nilikuwa naumwa lakini kuhusu ugonjwa hapana,”

Video hiyo ambayo ilisambaa mitandaoni ikimuonyesha mrembo huyo akiwa katika hali isiyokuwa ya kawaida ilizua taharuki kwa mashabiki wake.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW