Michezo

Wenger ajutia kukaa Arsenal kwa miaka 22 ‘Nilifanya makosa makubwa sana’

Wenger ajutia kukaa Arsenal kwa miaka 22 'Nilifanya makosa makubwa sana'

Aliyekuwa meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa makosa makubwa anayojutia kwenye taaluma yake ya ufundishaji soka ni kukaa kwa miaka 22 ndani ya timu hiyo.

Former Arsenal manager Arsene Wenger was interviewed by Christine Kelly on RTL

Wenger ameyasema hayo wakati alipokuwa akifanya mahojiano na chombo cha habari cha RTL hali iliyoshangaza watu wengi waliyokuwepo mahala hapo.

Wenger stepped down as Arsenal manager earlier this summer after 22 years at the helm

Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 68 ameeleza kuwa hajatambua bado atakwenda kufundisha klabu gani huku akisisitiza kamwe hatotumia muda mrefu kwenye kazi atakayofanya.

Alipoulizwa na Christine Kelly anadhani ni kosa gani kubwa alishawahi kufanya ndipo akajibu kuwa ni kukaa kwenye klabu moja kwa muda wa miaka 22.

”Kukaa ndani ya Gunners kwa muda wa miaka 22 ni kosa kubwa sana kwangu. Mimi ni mtu ambaye napenda kutoka sehemu moja kwenda nyingine lakini pia kukutana na changamoto,” amesema Wenger.

Arsene Wenger ameongeza ”Nilikuwa mfungwa wa changamoto zangu mwenyewe kwa wakati huo. Niliamua kuachana na Arsenal baada ya kujua kuwa kuna watu wengi wanao nizunguka wanaumia myoyo yao pamoja na familia yangu.”

Wenger ameipatia Arsenal mataji matatu ya ligi kuu ya Uingereza, saba ya FA Cup na kujenga historia iliyotukuka msimu wa mwaka 2003-04 kumaliza ligi bila kufungwa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents