Michezo

Wenger amkingia kifua Alexis Sanchez

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa kiwango cha chini kinachoonyeshwa na mchezaji wake, Alexis Sanchez tangu kuanza kwa msimu hakuusiani na taarifa za yeye kuhusishwa kuamia Manchester City.

Wenger amesema kuanza chini ya kiwango kwa Sanchez msimu huu hakuusiani kabisa na Man City bali ni kutokuwa na utimamu wa mwili baada ya kutoka katika matibabu.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Chile,Sanchez hajacheza dakika 90 katika michezo ya Ligi Kuu nchini Uingereza lakini alikuwa miongoni mwa wachezaji waliyo cheza dhidi ya Cologne michuano ya Europa League.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari baada ya mchezo dhidi ya Doncaster, Wenger aliulizwa kama Sanchez amebadilika tabia baada ya City kuhitaji kumsaini wakati wa majira ya joto.

“Alexis Sanchez amekuwa nje ya uwanja kutokana na majeraha, najaribu kumfanya arejee katika kiwango chake na kwangu mimi nadhani mashindano ya Europa League na League cup ni muhimu,” amesema Wenger.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents