Michezo

Wenger atangaza vita kurudi tena mzigoni, Asema anarejea mwezi January

Aweka wazi mpango wake wa kurudi tena kazini

Aliyekuwa kocha wa Arsenal Mfaransa Arsenal Wenger ambaye alitangaza kustaafu soka majira ya joto mwezi mei mwaka huu 2018 na nafasi yake kuchukuliwa na Mhispania ambaye aliitumikia klabu hiyo yenye maskani yake London nchini Uingereza ametangaza kurejea tena kazini.

Wenger amesema hayo na kusema kuwa “Naamini ntarejea tena mwezi Januari sinauhakika ntaanzia wapi ila najisikia kurudi na niko tayari kurejea tena”

Arsene Wenger ameelezea nia yake ya kurudi kwenye soka mwezi Januari baada ya kupokea ofa nyingi sana kutoka duniani kote.

Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 68 alimaliza utawala wake huko Arsenal msimu uliopita baada ya kukata tamaa kwa muda kutokana na kutokuwa na mafanikio makubwa katika klabu hiyo yenye maskani yake Emirates, lakini anahisi kuwa bado ana nguvu na yuko tayari kukabiliana na changamoto mpya.

“Ndani ya miaka yangu 22 niliyoitumikia Arsenal, nina uzoefu mkubwa katika viwango mbalimbali. Kuna maswali mengi sana kutoka duniani kote,” alisema Mfaransa huyo. “Kuna vyama, timu za kitaifa, inaweza kuwa Japan”.

“Ninaamini kwamba nitaanza tena Januari ,” alisema Wenger, ambaye alijiunga na Arsenal akitokea klabu ya Kijapani ya Nagoya Grampus Eight mwaka 1996.

Boss huyo wa zamani wa Gunners ilisemekana huenda akawa kocha mkuu wa Japan, na hivi karibuni kuna habari zilienea kuwa atajiunga katika bodi ya wababe wa Kifaransa PSG, lakini Wenger alielezea kwamba hajui ni jukumu gani atakalopata.

“Najisikia na kujiona kuwa nimepumzika vyakutosha na niko tayari kufanya kazi tena. Lakini ni wapi? Sijui bado.”

Wenger pia aliweza kuongelea suala la kiungo wa Arsenal Mesut Ozil kutokana na kile kilichotokea kwa kiungo huyo kutangaza kustaafu kuitumikia timu yake ya taifa ya Ujerumani kwa kile alichodai kuwa alionyeshewa vitendo vya ubaguzi kutoka kwa baadhi ya viongozi wa juu wa soka nchini Ujerumani na kusema;-

“Ninaamini kwamba Ujerumani bado wanumuhitaji Ozil, Natumaini kwamba kocha Joachim Low kocha mkuu wa Ujerumani anaweza kumshawishi na hatimae atarudi,” alisema Wenger.

“Ozil ni moja ya wachezaji bora mpira wa miguu, ambaye huwezi kusema hana umuhimu katika Kombe la Dunia. Sikumpenda kitendo cha kutoka timu ya kitaifa ya Ujerumani.”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents