Michezo

Wenger ni meneja bora katika historia ya soka- Antonio Conte

Arsene Wenger, ataendelea kukumbukwa  ” Ni miongoni mwa mameneja bora katika historia ya soka hata kama  Arsenal watapoteza katika mchezo wa fainali wa FA”, alisema bosi huyo wa Chelsea, Antonio Conte.

Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka, 67, amekuwa bosi katika kikosi cha Gunners  tangu mwaka  1996  na siku za hivi karibuni amekuwa na wakati mbaya zaidi ndani ya klabu ya Arsenal.

Wenger , alisema hatima yake ndani ya klabu hiyo itaamuliwa na kikao cha Bodi ambacho kitakaa baada ya mchezo wao wa fainali ya FA utakao wakutanisha Arsenal dhidi ya Blues.

Arsene Wenger, atakuwa kocha mwenye mafanikio zaidi kama atashinda kombe la  FA Cup kwa  kuifunga Chelsea katika mchezo wao wa Fainali. 

“Namfahamu sana , Arsene Wenger , amefanya mengi  mazuri katika  kombe la FA na kushinda mataji ,” alisema  Conte.

Conte, anaamini  Wenger  ataendelea kusalia ndani ya kikosi cha  Arsenal akiwa kama  meneja katika msimu ujao wa ligi.

“Sitaki kuamini kuwa huu ndio utakuwa mchezo wake wa mwisho ndani ya Arsenal, anastahili kuendelea kuitumikia Arsenal,” alisema Muitaliano huyo ambaye anafikiria kuchukua taji lake la pili katika msimu wake wa kwanza akiwa  Stamford Bridge baada ya kuchuku la ligi ya Uingereza.

 

“Wakati mwingine nafikiria kwa hapa nchini Uingereza  unakuwa na thamani  kama unapata nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa . Ni msimu huu tu  ndio haja pata nafasi ya kufuzu  kushiriki michuano hiyo, ila amefanya kazi kubwa ndani ya Arsenal”

“Ukiwa umeweza kukaa kwa muda mrefu ndani ya klabu hakika unastahili kuwa meneja bora wa kihistoria na atabaki kuwa hivyo.” alisema kocha wa Chelsea Antonio Conte.

Klabu ya  Chelsea haijashinda taji la FA Cup tangu ilipofanya hivyo kwa mara ya mwisho mwaka  2012 wakati wa kocha,  Roberto di Matteo na kuifunga Liverpool kwa jumla ya magoli 2 kwa 1 katika dimba la Wembley.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents