Michezo

Wenger: Tulicheza vizuri dhidi ya Barca

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema vijana wake walicheza vizuri katika uwanja wa Nou Camp licha ya kufungwa kwa magoli 3-1 na Barcelona Ligi ya Bingwa Ulaya.

3243BC9800000578-3496050-image-a-82_1458170093339

Arsenal walilazwa kupitia mabao ya Neymar, Luis Suarez na Messi. Bao lao la kufutia machozi lilifungwa na Mohamed Elneny.

Arsenal hawajafika hatua ya robofainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya tangu 2010. Arsene Wenger amesema

“Nafikiri tulicheza vyema, ulikuwa mchezo mzuri kati ya timu mbili nzuri. Tumeondolewa kwa masikitiko lakini wana ustadi wa hali ya juu hasa katika safu ya mashambulizi na ukifanya kosa kidogo tu safu yako ya ulinzi wanaweza kukuadhibu,” alisema Wenger baada ya mechi.

“Wakati muhimu katika mchezo huo ni mambo yalipokuwa 1-1 kwa sababu nilidhani walikuwa wanayumbayumba kiasi. Kama tungefunga bao la pili wakati huo badi mambo yangekuwa tofauti labda. Lakini hatukuweza.

“Katika michezo yote miwili, ukiangalia nafasi ambazo tuliunda, zilikuwa nyingi. Inauma kuondolewa kwenye michuano lakini tulicheza vyema sana dhidi ya timu ambayo labda ndiyo bora zaidi Ulaya.”

Arsenal walilazwa 2-0 mechi ya mkondo wa kwanza uwanjani Emirates, mabao yote yakifungwa na Lionel Messi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents