Habari

Wenyeviti serikali za Mitaa CUF waungana na Profesa Lipumba

Wenyeviti wa Serikali za Mitaa CUF Mkoa wa Dar es Salaam, wameungana na uamuzi wa Baraza Kuu la Uongozi upande wa Mwenyekiti wake anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba kuwatimua uanachama wabunge 8 Viti Maalum na Wabunge wawili.

Akizungumza na wanahabari jana kwa niaba ya wenzake 14, Mwenyekiti wa serikali ya Mitaa wa Keko Mwanga B, Shilingi Shilingi wanaunga mkono uamuzi wote wa Baraza Kuu la Uongozi kwa kuwa wabunge hao wamebainika kukihujumu chama hicho.

“Tunamtambua Maalim Seif Sharif Hamad kama katibu mkuu lakini kwa sasa nafasi yake inakaimiwa na Magadalena Sakaya kutoka na yeye kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya CUF,” alisema Shilingi

Wabunge waliotimuliwa CUF ni Raisa Abdallah Mussa, Khadija Salum Ally, Halima Ali Mohamed, Salma Mohamed Mwasa, Miza Bakari Haji, Riziki Shahari Mngwali, Saumu Heri Sakala na Severina Mwijage.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents