Michezo

West Ham kufanya mazungumzo na aliyekuwa kocha wa Man City, Manuel Pellegrini

Klabu ya West Ham United ya nchini Uingereza ipombioni kufanya mazungumzo na aliyekuwa meneja wa Manchester City, Manuel Pellegrini kuhusu kuitumikia timu hiyo.

Ripoti iliyopo hivi sasa ni kuwa raia huyo wa Chile, Pellegrini amesaini mkataba licha ya kuwa dili hilo bado halijakamilika.

Pellegrini mwenye umri wa miaka 64, amekuwa akiiongoza klabu ya Hebei China Fortune tangu mwaka 2016 inayoshiriki ligi kuu ya china maarufu kama Chinese Super League huku ikielezwa kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuziba nafasi ya  David Moyes.

Wakati meneja wa klabu ya Newcastle, Rafael Benitez bado akisalia kuwa mmoja wa wanao hitajika ndani ya kikosi cha West Ham.

Benitez raia wa Hispania amesaliwa na miezi 12 ndani ya Newcastle huku akiwa na nafasi ya kuuongeza mkataba wake.

Pellegrini amewahi kuiyongoza Manchester City kati ya mwaka 2013 na 2016 na kuiwezesha kushinda taji la ligi kuu nchini Uingereza kwenye msimu wake wa kwanza akiwa meneja wa timu hiyo.

Meneja huyo wazamani wa Real Madrid amewahi kuiwezesha City kufika hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya mwaka 2016 akiwa ni kocha pekee aliyeiwezesha timu hiyo kufika hatua hiyo kwenye historia mpaka sasa.

Mwenyekiti wa klabu ya Weste Ham, David Sullivan amepania kumtafuta kocha mwenye levo ya hali ya juu kimafanikio atakayo iwezesha timu yake kupiga hatua.

Miongoni mwawanao husishwa na kutua kwenye klabu hiyo ni pamoja na meneja wa klabu ya Shakhtar Donetsk, Paulo Fonsec.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents