Michezo

West Ham wamsimamisha kazi Tony Henry juu ya madai ya sera ya klabu dhidi ya kusaini Waafrika

By  | 

The Daily Mail imeripoti kwamba Tony Henry alisema wachezaji wa Afrika husababishia matatizo wakati wasipo kuwa na timu.

Katika taarifa hiyo, West Ham wamesema kamwe hawatoweza kuvumilia aina yoyote ya ubaguzi na walifanya uamuzi haraka kwa sababu ya hali mbaya ya madai hayo.

Chama cha Soka yaani FA kimesema kitashughulikia jambo hilo rasmi.

West Ham wamesema kwamba kwa sasa Henry amesimamishwa kazi huku akisubiri uchunguzi kamili na wa kina kufanyikia.

Klabu hiyo iliendelea kutoa taarifa kwamba Familia ya West Ham United ni ya umoja ambapo, haijali jinsia, umri, uwezo, rangi, dini au mwelekeo wa kijinsia, kila mtu anakaribishwa.

“Klabu hiyo haitatoa maoni tena mpaka uchunguzi umekamilika na Wafanyakazi wote wamefunzwa juu ya usawa, utofauti na upendeleo usio na ufahamu. Ilisema klabu hiyo.”

Chama cha Soka kililisema kwamba jambo hilo “limewashtusha”.

West Ham wana wachezaji sita wenye asili ya kiafrika katika kikosi cha kwanza ya timu hiyo ambao ni Cheikhou Kouyate, Pedro Obiang, Joao Mario, Angelo Ogbonna, Arthur Masuaku na Edimilson Fernandes.

Mshambuliaji wa Senegal Diafra Sakho aliondoka kwenye klabu hiyo katika dirisha la Januari kujiunga na Rennes, na huku Andre Ayew wa Ghana akielekea Swansea.


Aliposti mchezaji Cheikhou Kouyate

West Ham wanashika nafasi ya 12 katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Henry, ambaye hapo awali alifanya kazi kwenye timu mbalimbali kama Everton, Sunderland na Chelsea, alijiunga na West Ham mwaka 2014. Alichezea klabu kadhaa ikiwa ni pamoja na Manchester City, Bolton na Oldham.

Na Raheem Rajuu

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments