Michezo

West Ham yamtimua kazi kocha wake Slaven Bilic

Klabu ya West Ham inayoshiriki ligi ya Uingereza imemuachisha kazi meneja wa timu hiyo, Slaven Bilic pamoja na benchi zima la ufundi kufuatia matokeo mabovu waliyopata dhidi ya Liverpool siku ya Jumapili.

West Ham hapo jana ikiwa chini ya Bilic ilikubali kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Liverpool katika Uwanja wa London.

Habari kutoka ndani ya klabu ya West Ham zinasema kuwa imefikia maamuzi hayo ili kusonga mbele na kutimiza malengo waliyojiwekea.

Kufuatia tamko hilo la klabu ya West Ham hivyo meneja Bilic, na wasaidizi wake Nikola Jurcevic, Edin Terzic, Julian Dicks na Miljenko Rak wataachana na timu hiyo.

“Klabu imeamua kutafuta kocha mpya atakaeweza kuipeleka West Ham United mbele zaidi ya hapa alipoifikisha Bilic,” habari kutoka ndani ya klabu West Ham ilieleza.

Wagonga nyundo hao wa Uingereza wameshinda michezo miwili pekee na kupoteza mitatu msimu huu wa mwaka 2017/18.

Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya mchezo wao na Liverpool, Bilic amesema “Presha imezidi kuwa kubwa mchezo hadi mchezo na sasa hali imekuwa kubwa zaidi.”

Bilic ameongeza “Sionekani kama mtu niliyekata tamaa hapana kwa upande mwingine hali ya ndani ya klabu ya West Ham siyo nzuri.”

“Siwezi kuzungumzia ubaya wowote juu ya wamiliki wa klabu wamekuwa wakionyesha mchango wao mkubwa na niwatu wazuri sana kwangu kwa msimu  mmoja na nusu niliyokuwa hapa lakini hali nimbaya.”

West Ham watashuka Uwanjani siku ya Jumapili ya Novemba 19 kukabiliana na Watford.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents