Soka saa 24!

Weusi yageuka Kampuni

Nikki_mfalme

Mkali wa staili Nikki wa pili, amesema kuanzia sasa Weusi itakuwa kampuni na kuitwa Wausi Entertaiment ambayo itakuwa inashughulika, na kuandaa matamasha, mikataba, na kusiamamia kazi za wasanii wa kundi hilo.

Amesema yeye atakuwa kama msemaji mkuu wa kundi hilo, na taarifa zote zitakazokuwa zinahusiana na kundi hilo, basi yeye ndiye anayepaswa kuulizwa na kujibu. Pia ameeleza kwamba weusi wenyewe wanaundwa na makundi mawili kutoka Arusha, likiwemo River Camp Solders, na Nako 2 Nako Solders.  Kundi hilo pia limekusanya wasanii wa makundi hayo mawili wakiwemo, Lord Eyes, G nako, G gwarawara, Joh Makini, Nikki wa pili na wasanii wengine wa makundi hayo.

Kundi kwa sasa linatarajia kuachia ngoma nyingi kutoka kwa wasanii hao, ambazo miongoni mwake zitatoka kuanzia ijumaa hii, hivyo msemaji wa WEUSI, anasema mkae mkao wa kula kwani ujio huu ni wa nguvu zaidi.

Amesema ujio wao wa sasa ni kutoa video ya Kiujamaa katika wiki hii,  wimbo wa Bey bey wa Joh Makini, video ya Pleyer ya Nikki wa pili ambayo imegonganisha mikono miwili ya Marco Chali na Narealy aliyewahi kuingiza mkono wake kwenye wimbo wa Kiujamaa.

Contiouns………

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW