Habari

Wezi hawa wachukuliwe hatua kali!

PiracyKuna kila sababu ya kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote ambao wanatumia muda wao mwingi kutafuta nyimbo za wasanii wa kibongo na kuziuza kinyume na sheria kwa njia mbali mbali ambazo kila kukicha wanazibuni, kwani kulingana na hali ilivyo kwa sasa unaweza kujipatia albam ya msanii yoyote bila kutumia gharama zozote…

PiracyKuna kila sababu ya kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote ambao wanatumia muda wao mwingi kutafuta nyimbo za wasanii wa kibongo na kuziuza kinyume na sheria kwa njia mbali mbali ambazo kila kukicha wanazibuni, kwani kulingana na hali ilivyo kwa sasa unaweza kujipatia albam ya msanii yoyote bila kutumia gharama zozote labda kitakachokugharimu ni cd ya sh 500/= jambo ambalo si zuri kwani wasanii wanapiga kazi ili waweze kunufaika na kazi zao lakini anatokea mtu anakula kwa ubua kwa kweli inaboa sana.

 

 

 

Ukijaribu kuchunguza karibu kila stationary pamoja na video Library nyingi za hapa jijini utakuta wanarekodi nyimbo na bei imeandikwa kwa kila cd kana kwamba biashara wanayoifanya ni ya halali kwa kweli kitendo hiki kinatakiwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria au hao wanaojiita wasimamia haki za wasanii watoe tamko kuhusiana na hili na kama wanachukulia poa pia ijulikane.

 

 

 

Cha kufurahisha zaidi si kama wasanii wenyewe hawalioni hili sema wameamua kulifumbia macho kwani kwa namna moja au nyingine yawezekana wakawa kuna manufaa ambayo wanayapata kupitia sehemu hizo za biashara, ila itakuwa vema sana iwapo wataamua kulivalia njuga suala hili huku wakifikiria machungu, sumbufu na gharama wanazoingia wawapo katika harakati za kurekodi kisha atokee mtu ambaye hajatoa ushirikiano wowote zaidi ya kuuza tena kwa bei rahisi ile kinoma…Inauma Aisee.

 

 

 

Ona sasa..wale ambao si wasanii na ni wanunuzi wazuri katika maeneo hayo ambayo biashara hiyo huendelea ndio wa kwanza utawasikia wakisema “Mh kwa mpango huu msanii wa kibongo ataendelea vipi? Mwandishi wa Bongo5 aliweza kuyanasa maneno hayo kwenye duka moja la kanda lililopo maeneo ya Mwenge ambapo lilionekana kujaza raia ambao walikuwa na vijikaratasi vyao vyenye list ya nyimbo wanazotaka.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents