Habari

Wezi waiba gauni la Lupita Nyong’o alilovaa kwenye tuzo za Oscars 2015 lenye thamani ya shilingi milioni 274

Gauni la muigizaji wa Kenya, Lupita Nyong’o lenye thamani ya $150,000 (zaidi ya shilingi milioni 274) la Calvin Klein alilolivaa kwenye tuzo za Oscars wiki iliyopita limeibiwa, polisi wamesema jana.

Lupita-Nyongo-Oscars-2015-Pictures

Gauni hilo lililotengenezwa maalum kwaajili yake lilikuwa limezungushiwa vigolori 6,000 vya rangi nyeupe. Liliibiwa kwenye chumba chake cha London Hotel iliyopo West Hollywood mchana, amesema msemaji wa LAPD county ya West Hollywood.

lupita-nyongo-oscars-2015-2

“Ms Nyong’o hakuwemo chumbani wakati wizi huo ukifanyika,” Deputy John Mitchell ameliambia shirika la habari la Uingereza, Reuters.

jk-simmons-lupita-nyongo-oscars-2015-1

Gauni hilo la Calvin Klein lililobuniwa maalum na designer Francisco Costa lililimfanya Lupita kuwa miongoni mwa mastaa waliopendeza zaidi kwenye red carpet ya tuzo hizo zilizofanyika Jumapili iliyopita.

Nyong’o aliiambia Reuters kuwa alisaidia pia kubuni gauni hilo la kipekee lililokuwa influenced na bahari.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents