Technology

WhatsApp haitofanya kazi kwenye simu hizi hadi mwishoni mwa mwaka huu

Kama unatumiA smartphone ya kizamani kutuma ujumbe wa WhatsApp, jipange kununua ya kisasa sababu unaweza usiweze tena kufurahia huduma hiyo.

1bac1fac00000578-3469210-image-a-25_1456745204816

WhatsApp imetangaza kuwa haitofanya kazi tena kwenye baadhi ya simu za kizamani hadi mwishoni mwa mwaka huu. App hiyo imetangaza kutozisupport tena zimu zinazotumia mifumo ya zamani ya Windows, Android na Apple hadi January, na Blackberry na Nokia hadi kufikia katikati mwa 2017.

Ni kwasababu simu za kizamani, hazitoweza kukubali mabadiliko yatakayoongezeka kwenye app hiyo. WhatsApp imetoa tangazo hilo wakati ikisherehekea kutimiza miaka 7 tangu ianze kufanya kazi mwaka 2009.

App hiyo kwa sasa inatumiwa na watu zaidi ya bilioni 1 duniani.

Kupitia blog yake, WhatsApp imetaja simu itakazoziacha kuwa ni pamoja na zinazotumia mfumo wa Android 2.1 na Android 2.2; Windows Phone 7 na iPhone 3GS/iOS 6. Na hadi June 2017, WhatApp haitopatikana kwenye BlackBerry 10; Nokia S40; na Nokia Symbian S60.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents