Technology

WhatsApp kuja na ‘version’ rasmi ya kwenye computer

Najua kuwa kwa sasa unaweza kutumia WhatsApp kwenye computer yako kwa kuscan code maalum na kuunganisha app ya simu na whatsapp web. Lakini siku zijazo, utaweza kutumia WhatsApp ya kwenye computer inayojitegemea yenyewe, imebainika.

whatsapp-730x365

Kuna tetesi kuwa WhatsApp itakuja kwenye desktop kwa computer za Mac na Windows katika nia ya kujipanua zaidi. WhatsApp ya kwenye computer itakuwezesha kupiga simu za sauti na video na huduma zingine.

Ikianza, hautakuwa na haja tena ya kuscan QR code kujiunganisha na browser yako. Hatua hii itakuwa huduma mbadala wa huduma kama Slack, Messenger au Skype kwa mawasialino yasiyo kuwa ya maandishi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents