Technology

WhatsApp waruhusu video za Youtube kucheza kwenye programu yao

Baada ya muda mrefu WhatsApp kutangaza kuwa itafanya maboresho makubwa matano kwa mwaka huu tayari, Program hiyo imeanza maboresho hayo kwa kuanza kuruhusu video za YouTube kucheza moja kwa moja kwenye Programu wezeshi yao.

Program hiyo ilianza kuruhusu kwanza kwa watumiaji wa iOS mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu lakini kwa sasa imeruhusu kwa watumiaji wa Android ambapo mtumiaji kama bado hujaona maboresho hayo itakubidi u-update kifaa chako ili uweze kupata huduma hii mpya.

Awali WhatsApp ilikuwa inaruhusu link tu kwenye programu hiyo ambapo mtumiaji alikuwa analazimika kubofya Link na kupelekwa moja kwa moja kwenye App ya YouTube.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents