Afya

WHO “Dawa ya Corona anayopendekeza Trump Hydroxychloroquine ni hatari kiafya”

Majaribio yanayofanyiwa dawa ya ugonjwa wa malaria Hydroxychloroquine ili kuona iwapo inaweza kutibu virusi vya corona yamesitishwa kutokana na hofu ya usalama wake, shirika la afya duniani WHO limesema.

Vipimo vilivyokuwa vikifanywa katika mataifa kadhaa vimesitishwa kwa muda kama hatua ya kuchukua tahadhari, lilisema shirika hilo siku ya Jumatatu.

Hatua hiyo inajiri baada ya utafiti wa tiba uliofanyika hivi karibuni kusema kwamba dawa hiyo inaweza kuongeza hatari ya mgonjwa kufariki kutokana na virusi hivyo.

Rais Donald Trump amesema kuwa anatumia dawa hiyo kuzuia virusi hivyo.

Rais huyo wa Marekani ameikuza dawa hiyo ya malaria, kinyume na ushauri wa kimatibabu na onyo kutoka kwa maafisa wa Afya kwamba inaweza kusababisha tatizo la moyo.

US President Donald Trump speaking at the White HouseRais Trump alizungumzia kabla kuhusu matumizi ya dawa hizi kwa ajili ya Covid-19

Kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins vifo vilivyotokana na corona vimefikia 98,218.

Wiki iliopita, utafiti uliofanywa na jarida la tiba duniani Lancet ulibaini kwamba hakuna faida yoyote kwa kutumia dawa ya Hydroxychloroquine na kwamba utumizi wake unaweza kuongeza idadi ya vifo miongoni mwa wagonjwa hospitalini walio na maambukizi ya corona.

Hydrochloroquine ni dawa salama ya kutibu ugonjwa wa malaria, baridi yabisi na Lupus, lakini hakuna majaribio yoyote ambayo yamependekeza matumizi yake kutibu Covid-19.

Watafiti wanasemaa kwamba wagonjwa wa Covid-19 hawafai kutumia hydroxychloroquine.

Shirika la Afya duniani linafanyia majaribio dawa kadhaa kuona iwapo zinaweza kutibu ugonjwa huo mbali na kuripoti kwamba baadhi ya watu binafsi wamekuwa wakitumia dawa hiyo na hivyobasi kujisababishia madhara makubwa.

Watafiti wanasema wagonjwa wa Covid-19 wasitumie dawa ya hydroxychloroquine nje ya majaribio ya tibaWatafiti wanasema wagonjwa wa Covid-19 wasitumie dawa ya hydroxychloroquine nje ya majaribio ya tiba

Siku ya Jumatatu, maafisa katika shirika hilo la Umoja wa Mataifa walisema kwamba hydroxychloroquine itaondolewa katika majaribio hayo kwa muda ili kuruhusu uchunguzi wa usalama wake.

Utafiti huo wa Lancet ulihusisha wagonjwa 96,000 wa virusi vya corona ambapo kati yao 15,000 walipatiwa dawa ya Hydroxychloroquine ama ile inayohusishwa na Chloroquine , pekee ama na dawa ya antibiotic.

Utafiti huo ulibaini kwamba wagonjwa hao walikuwa na hatari kubwa ya kufariki hospitalini na kupatwa na tatizo la moyo ikilinganishwa na wagonjwa wengine wa Covid-19.

Hatari ya mgonjwa anayetumia hydroxychloroquine kufariki ilikuwa asilimia 18, asilimia 16.4 kwa waliotumia Chloroquine na asilimia 9 kwa kundi jingine.

Wale waliotibiwa na hydroxychloroquine au chloroquine kwa mchanganyiko na dawa ya antibiotic walikuwa na hatari ya juu zaidi kufariki. Watafiti hao walionya kwamba Hydroxychloroquine haifai kutumiwa kando na majaribio hayo.

Chanzo BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents