Afya

WHO yasema bado kuna safari ndefu kuimaliza corona, Ndani ya saa 24 maambukizi zaidi ya 106,000

MKuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameonya kwamba janga virusi vya corona bado ni safari ndefu licha ya kwamba wanaoathirika wanaendelea kuongezeka kote duniani kila uchao.

WHO imesema kwamba waathirika wapya 106,000 wameripotiwa katika shirika hilo ndani ya kipindi cha saa 24 zilizopita.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ameonesha wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa maambukizi katika mataifa ya kipato cha chini na cha wastani.

Onyo hilo linawadia huku idadi jumla ikikaribia kufika milioni tano.

Idadi hiyo ya kusikitisha inafikiwa chini ya wiki mbili baada ya ya kurekodiwa maambukizo milioni nne kote duniani.

Wataalamu wameonya kwamba idadi kamili ya maambukizi huenda ikawa ya juu zaidi na idadi ya wanaopimwa ni ya chini katika nchi nyingi ambazo wanaficha taarifa zao.

Zaidi ya watu 326,000 wanakadiriwa kuwa wamekufa kwa virusi vya corona kote duniani kulingana na chuo kikuu cha Johns Hopkins.

Marekani bado ndio iliyoathirika zaidi ikiwa na walioambukizwa milioni 1.5 na idadi ya waliokufa ikifikia 92,000.

WHO imesema nini?

“Katika kipindi cha saa 24 zilizopita, kumekuwa na maambukizo mapya 106,000 ambayo yameripotiwa kwa WHO – ambayo ni makubwa zaidi kuandikishwa kwa siku moja toka janga la corona lianze,” Dkt Tedros aliwaeleza wanahabari Jumatano jioni.

“Karibia theluthi mbili ya walioathirika wameripotiwa katika nchi nne pekee,” aliongeza.

 

Dkt. Tedros baadae alionya kwamba dunia kwamba safari ya kupambana na janga hili bado ni ndefu.

Onyo lake linawadia wakati ambao mataifa kadhaa kama vile Marekani imeanza kulegeza masharti.

This handout image provided by the World Health Organization (WHO) on May 18, 2020Dkt Tedros aonya kuwa bado kuna safari ndefu kwa dunia kuimaliza corona

Dkt. Mike Ryan, mkurugenzi wa masuala ya dharura wa WHO, pia alizungumza na wanahabari dhidi ya matumizi ya dawa za malaria ya chloroquine na hydroxychloroquine zinazohusishwa na ugonjwa wa Covid-19.

Hilo linawadia baada ya Rais Trump kusema amekuwa akinywa dawa ya inayokusudiwa kutibu malaria kama njia moja ya kujikinga dhidi ya virusi vya corona, licha ya onyo kutoka kwa maafisa wake wa afya kuhusu matumizi ya dawa hiyo.

 

“Hadi kufikia sasa, dawa ya kutibu malaria ya hydroxychloroquine au chloroquine bado haijathibitishwa kuwa salama katika kutibu ugonjwa wa Covid-19 kama njia ya kukabiliana na ugonjwa huo,” Dkt. Ryan amesema.

” Na ukweli ni kwamba, mamlaka nyingi zimetoa onyo ya athari zinazoweza kutokea kwa matumizi ya dawa hii.”

Licha ya wasiwasi huo, wizara ya afya ya Brazil imetoa mwongozo mpya Jumatano kuidhinisha matumizi ya dawa hizo mbili wakati maambukizo ya virusi vya corona yanaendelea kuongezeka.

Brazil kwa sasa ina waziri wa tatu wa afya katika kipindi cha wiki kadhaa baada ya wawili waliotangulia kuhitilafiana na Rais Jair Bolsonaro juu ya namna ya kushughulikia mlipuko wa virusi hivyo.

Taifa hilo kwa sasa lina maambukizi zaidi ya 270,000 ya ugonjwa wa Covid-19 ikiwa ni ya tatu kwa kupata maambukizi mengi duniani, huku wengine karibia 20,000 wakithibitishwa Jumatano pekee.

Wataalamu wameonya kwamba maambukizi nchini humo bado yako mbali kufikia kilele chake na kuna wasiwasi mkubwa kuhusu kusambaa kwa haraka kwa virusi katika maeneo duni na jamii za wenyeji.

Katika taarifa nyengine:

  • Waziri wa afya wa Bolivia amekamatwa kwa madai ya kuhusishwa na ufisadi katika ununuzi wa mashine za kupumua kwa bei ya juu zaidi zinazokusudiwa kutumiwa kwa wagonjwa wa virusi vya corona
  • Kimbunga kikali kimekumba mashariki ya India na kusababisha maporomoko huko Bangladesh lakini hatua za kudhibiti virusi vya corona zinafanya suala la kuhamia maeneo salama na utoaji wa chakula cha msaada kuwa changamoto
  • Sweden imetangaza kupitia tena suala la makazi ya kutunza wazee juu ya hofu kwamba kuna baadhi ambayo hayana oksijeni ya kutosha kwa wagonjwa
  • Maafisa wa Ugiriki wanasema wanatarajia kufungua tena sekta ya utalii mwezi ujao licha ya jenga hili linalokumba dunia
  • Nchini Uhispani, itakuwa ni lazima kuvaa barakoa pale ambapo haiwezekani kuchukua hatua ya kutokaribiana kuanzia Alhamisi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents