Tupo Nawe

Wilder baada ya kupokea kipigo kutoka kwa Fury atemana na kocha wake baada ya kurusha taulo ulingoni “Nilivalishwa mavazi mazito kg 18, Miguu ilichoka”

Wilder baada ya kupokea kipigo kutoka kwa Fury atemana na kocha wake baada ya kurusha taulo ulingoni "Nilivalishwa mavazi mazito kg 18, Miguu ilichoka"

Bondia Mmarekani Deontay Wilder ameamua kutemana na mkufunzi wake au mwalimu wake (Kocha) Mark Breland baada ya kupoteza pambano lake dhidi ya Muingereza Tyson Fury.

Kupitia ukurasa wa Twitter wa Boxing Kingdom umeripoti kutokea kwa taarifa hizo.

Hii imekuja baada ya mwalimu huyo wa muda mrefu kurusha taulo uwanjani ili kumtaka mwamuzi asitishe pambano hilo kwenye raundi ya 7 ambapo ilionekana Wilder kuzidiwa na mwisho wa pamabno hilo Wilder alipoteza ubingwa wa WBC kwa TKO dhidi ya Tyson Fury.

Mbali na hilo , imeelezwa Wilder amejieleza kwamba mavazi yake ambayo aliyavaa wakati akiingia ulingoni usiku ule wa pambano lake dhidi ya Tyson Fury ndio chanzo cha kupoteza pambano hilo. Amesema vazi lile lilikuwa na uzito wa Kilo 18, hivyo lilichosha miguu yake na kupelekea kupokea kichapo hicho kwa TKO.

“Hakuniumiza hata kidogo, lakini ukweli rahisi ni kwamba sare zangu ndio zilikuwa nzito sana kwangu,” Wilder alimwambia Yahoo Sports. “Sikuwa na nguvu miguuni tangu mwanzoni mwa pambano. Katika mzunguko wa tatu, miguu yangu ilipigwa kama na butwa hivi. Lakini mimi ni shujaa na watu wanajua kuwa mimi ni shujaa. ”

“Watu wengi walikuwa wakiniambia: ‘inaonekana kana kwamba kuna kitu hakipo sawa kwako’ lakini kumbe kweli, lakini wakati upo jukwaani unatakiwa kusahau kila kitu, Nilijaribu sana kufanya kila jambo lakini  Nilijua fika sikuwa na nguvu miguuni kwa sababu ya sare zangu, ” – Maneno ya Wilder

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW