Habari

Will Smith: Nina bahati Jada kuwa mke wangu


Will Smith amemsifia mke wake Jada Pinkett kwa kuifanya familia yake kuwa pamoja.

Muigizaji huyo wa Men In Black III na mke wake muigizaji wa series ya Hawthorne wana miaka 17 tangu waoane licha ya hivi karibuni kuwepo na fununu kuwa ndoa yao ipo matatani kuvunjika.

“Nina bahati sana kuwa na mtu kama Jada. Ni mwanamke wa pekee, mke na mama… ni mgumu kwakweli, yaani ni kama vile huwa hashtushwi na uzito na pressure za maisha, “ Will ameliambia jarida la People.

“Ni mtulivu sana na huchukulia rahisi kila hali. Anaweza kuvumilia lolote na napenda sana hilo kutoka kwake. Huwa tunaweka jitihada za kuitanguliza familia kwanza. Kuwepo kwa ajili yetu sote na kuwa karibu na watoto wetu ni jambo muhimu. Nachukulia serious sana suala la kuwa mzazi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents