Willian kutua Arsenal, Aubameyang kumwaga wino

Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre -Emerick Aubameyang, 31, anakaribia kutia saini mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo.. (Telegraph – subscription only)

Pierre-Emerick Aubameyang

 

Winga wa Chelsea na Brazil Willian 31, amekubali kutia saini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Arsenal utaogharimu paundi 100,000 kwa wiki. (ESPN)

Willian and Pedro

Lazio wana imani ya kukamilisha usajili wa kiungo wa kati wa Manchester City David Silva. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 atakuwa mchezaji huru mwisho wa msimu huu. (Sky Sports)

Barcelona inajiandaa kuwasilisha dau la paundi milioni 35.9 kwa beki wa Leicester mwenye umri wa miaka 24 raia wa Uturuki Caglar Soyuncu. (NTV Spor – in Turkish)Jesse Lingard

Jesse Lingard

Manchester United itasikiza ofa za kumuuza kiungo wa kati wa England Jesse Lengard mwenye umri wa miaka 27 . (Guardian)

West Ham haijapokea ombi la kumuuza beki wa kati wa England mwenye umri wa miaka 21 Declan Rice, kulingana na meneja.

Tottenham itaanza kumuangazia mshambuliaji wa England na Bournemouth mwenye umri wa miaka 28 Callum Wilson. (Express

Leeds imejiandaa kuwasilisha ofa ya kumsajili winga wa Brentford na Algeria Said Benrahma mwenye umri wa miaka 24. (Telegraph – subscription only)

Everton inamlenga beki wa Manchester United na Ureno 21 Diogo Dalot. (Star)Nahodha wa zamani wa Chelsea John Terry

Nahodha wa zamani wa Chelsea John Terry

Naibu mkufunzi wa Aston Villa John Terry ameorodheshwa katika kuchukua nafasi ya ukufunzi wa klabu ya Bournemouth ilio wazi. (Metro)

Klabu mpya ilioteuliwa katika ligi kuu, Leeds United wanapanga uhamisho wa mshambuliaji wa Argentina na Stuttgart Nicolas Gonzalez 22 utaogharimu £20m. (Mirror)

Manchester United walikuwa na hamu ya kumsajili beki wa Uholanzi Nathan Ake ,25, kabla ya kujiunga na Manchester City kutoka Bournemouth wiki hii.. (Sky Sports)

Bournemouth imekataa ombi la dau la £12m kutoka Sheffield United kumuuza kipa wa England Aaron Ramsdale mwenye umri wa miaka 22. (Sky Sports)Ainsley Maitland-Niles was injured during Arsenal's 0-2 defeat to Manchester City on the opening day of the 2018/19 season

Maitland-Niles, anayeweza kucheza kama beki na kiungo wa kati vilevile

Arsenal imetangaza kwamba iko tayari kumuuza kiungo wa kati wa England Ainsley Maitland-Niles, 22, . (Mirror)

Beki wa Bayern Munich na Ujerumani Jerome Boateng anasema kwamba hatosema hawezi kurudi katika ligi ya Premia. mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alihudumu msimu wa 2010-11 akiichezea klabu ya Manchester City. (Guardian)

Leeds inataka kumsaini beki wa kushoto wa Rangers na Croatia mwenye umri wa miaka 27 Borna Barisic. (Football Insider)

Leeds imewasilisha dau la £400,000 kwa kinda wa Fulham na England Cody Drameh ,18 ambaye hajashirikishwa katika kikosi cha kwanza cha Fulham . (Mail)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW