The Trio watoa wimbo wa kusherehekea siku ya wanawake duniani – Pambo

TRIO FINAL 2

Kundi la kinadada watatu kutoka Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT), The TRIO, wametoa wimbo wao mpya unaoitwa, ‘PAMBO’ ambao ni maalumu kwa ajili ya kuadhimisha siku ya wanawake duaniani.

Kundi hilo ambalo limekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu kidogo, sasa limeamua kutoa wimbo huo ikiwa ni maandalizi ya ujio wao kamili mwishoni mwa mwezi huu. Pamoja na wimbo huo, The TRIO pia wametoa video ya live performance ya wimbo wao wa ‘FALL IN LOVE’ ambayo ilirushwa kwa mara ya kwanza kwenye vituo vya runinga wakati wa sherehe za Valentine mwaka huu.

Kundi hilo linaundwa na kinadada watatu machachari, Angella Karashani (Malaika), Alice Kibopile (Alice) na Khadija Maige (Kadja). Wimbo umerekodiwa studio ya Surround Sound, chini ya mtayarishaji Ema The Boy.

Download Hapa

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents