Michezo

Winga aliyewanyanyasa Yanga na Simba

Klabu ya Mtibwa Sugar msimu huu imefanya usajili wa wachezaji wapya nane huku wengine wakipandishwa kutoka timu ya vijana ya wana tam tam, mchezaji wa kwanza kutia saini katika karatasi za usajili alikua ni Salum Ramdhani Kihimbwa ambaye ni mwenyeji wa mji kasoro bahari Morogoro.

Kihimbwa linaweza likawa jina geni kwa baadhi ya watu lakini kwa wale wanaofuatilia michezo ya wana tam tam msimu huu wa 2017/18 watakuwa wanatambua kipaji halisi cha winga huyo mwenye vitu adimu uwanjani kasi kubwa na chenga za maudhi ndo silaha kubwa ya kijana huyu.

Salum Ramdhani Kihimbwa maarufu kama Chuji amesema kuwa alipokea ofa nyingi za kujiunga na timu mbali mbali za ligi kuu lakini aliamua kuja Mtibwa.

“Nilipokea ofa nyingi za kwenda timu mbali mbali za ligi kuu lakini walipokuja Mtibwa Sugar sikutaka kujiuliza mara mbili hivyo niliamua kujiunga nao nikiamini itanifikisha mbali na kuendeleza kipaji changu na kunifanya niwe mchezaji mkubwa nikiamini  ‘style’ ya uchezaji wa timu hii utanifaa,” amesema Kihimbwa.

Salum Kihimbwa kulia akiwania mpira na Ally Shomary wa Simba

Msimu uliyopita, Kihimbwa alikuwa akikipiga katika  timu ya daraja la kwanza Police Moro na kudumu nayo kwa misimu mitatu mchezaji huyo alipofanyiwa mahojiano na mtandao wa klabu hiyo kama anaona utofauti wowote amesema.

“Sijakutana na ugumu wowote kwakuwa walimu wa Mtibwa Sugar wamenijenga kisaikolojia na kimazoezi hivyo kila niki ingia uwanjani nakua najiamini na kikubwa najitahidi sana mazoezini na kusikiliza maelekezo ya makocha wetu hivyo naweza kusema kuwa sina hofu na ligi kuu.”

SalumRamadhani Kihimbwa maarufu kama Chuji msimu huu amepachikwa jina la mvunja nyonga na mashabiki wa wana tam tam kutokana na chenga zake za maudhi zinavyowalambisha nyasi mabeki wa timu pinzani, Mvunja nyonga huyo amezungumzia kikosi cha Mtibwa Sugar na matarajio ya msimu huu 2017/2018.

“Kwanza kabisa tunamshukuru Mwenyezi Mungu msimu huu tumeanza ligi vizuri na kikubwa tulichokubaliana ni kushinda kila mchezo wetu hivyo kila mmoja wetu anapigana kuona linawezekana maana tuna kikosi kipana na bora kabisa cha kupambana na timu yeyote msimu nadhani hatujaja kusindikiza tumejiandaa kufanya vizuri sana kikubwa waamuzi wachezeshe kwa usawa tu na kila timu ipate inachostahili.”

Mchezaji huyo amesema kuwa hakuna beki aliyempa shida ila anaamini wote ni wazuri na amejipanga kawa kufanya mazoezi zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents