Michezo

Winga aliyewanyanyasa Yanga na Simba yupofiti kuikabili Azam FC Jumatatu

Mtibwa Sugar wanataraji kushuka dimbani Jumatatu hii Uwanja wa Azam Complex Chamazi majira ya saa 1:00 jioni kuwakabili Azam FC katika mchezo wa ligi kuu bara VPL huku wakiwa na winga wao machachari, Salum Ramdhani Kihimbwa aliyekuwa akisumbuliwa na majeraha.

Wana tam tam hao wanaelekea katika mchezo huo wakiwa na hali nzuri katika kikosi chao na mtandao rasmi wa klabu www.mtibwasugar.co.tz  umezungumza na mmoja wa meneja wasaidizi wa timu hiyo Amir na  kuelezea ujio wa Kihimbwa.

“Kwa sasa vijana wote wako sawa hatuna majeruhi wapya, Kihimbwa aliyekuwa na majeraha madogo naye karejea mazoezini na anaendelea kufanya vizuri, wapenzi wa Mtibwa Sugar waje kwa wingi jijini Dar es laam kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Azam “Amir

Winga aliyewanyanyasa Yanga na Simba

Winga huyo mwenye vitu adimu uwanjani kasi kubwa na chenga za maudhi ndo silaha kubwa ya kijana huyu anakumbukwa hasa namna alivyoweza kuzinyanyasa ngome za klabu kongwe nchini Simba SC na Yanga SC wakati alipocheza nazo.

Mtibwa Sugar yenye maskani yake mji kasoro bahari Morogoro inashika nafasi ya nne katika msimamo baada ya kukusanya pointi 17 katika michezo 10 ya ligi kuu bara(Vodacom Premier League) huku wapinzani wao Azam wakiwa nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu bara baada ya kukusanya alama 22.

Mchezo huo unataraji kuwa mkali na wenye ushindani kutokana na ubora wa vikosi vyote viwili , Kikosi cha wana tam tam kinaonekana kuimarika zaidi baada ya winga wake machachari Salum Kihimbwa kurejea baada ya kupona maumivu ya nyama za paja yaliyokuwa yakimsumbua.

Msimu uliopita katika ligi kuu bara vikosi hivi vilitoka sare katika michezo yote miwili, wa kwanza uliochezwa Azam Complex ulimalizika 1-1 na ule uliochzwa Manungu ulimalizika kwa sare ya 0-0.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents