Michezo

Winga wa Everton FC inayodhaminiwa na SportPesa asajiliwa Barcelona

Klabu ya Barcelona imethibitisha kumsajili tena winga Gerard Deulofeu kutoka Everton baada ya kutengua kipengele kilichowekwa wakati anauzwa kwamba Barcelona watakuwa na nafasi ya kumnunua tena ( buy-back clause ).

Mchezaji wa klabu ya Everton FC na timu ya taifa ya Hispania anayejiunga na Barcelona, Gerard Deulofeu

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Hispania chini ya miaka 21 hakuwepo kwenye mipango ya msimu ujao ya kocha Ronald Koeman katika klabu ya Everton, na msimu uliopita alicheza kwa mkopo  AC Milan.

Deulofeu alinunuliwa akitokea Barca kwenda Everton kwa dau la Euro milioni 6 kipindi cha majira ya joto na sasa akirudi kwa dau la Euro milioni 12 huku Everton ikiweka masharti, mchezaji huyo kutouzwa mpaka msimu mmoja utakapo malizika kwa wababe hao wa soka wa Hispania na endapo watamuuza ndani ya klabu hiyo kabla hajamaliza msimu mmoja wenyeji hao wa Goodson Park watahitaji asilimia kadhaa za mauozo ya mchezaji huyo.

Mkataba wa Deulofeu na Barcelona utamalizika mwaka 2019.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents