Burudani

Wivu wa kimapenzi watajwa kumng’oa msanii MJ Records, Nay wa Mitego ahusishwa

Producer Daxo Chali ambaye anafanya kazi zake katika studio za MJ Records hapo juzi alitangaza kuacha kumsimami msanii Nini kupitia studio hiyo, lakini stori za sasa zinadai chanzo cha hilo ni wivu wa kimapenzi.

Nini na Haitham

Daxo Chali alikuwa akiwasimamia Haitham na Nini ambaye inadaiwa kuwekwa pembeni. Hiyo juzi kupitia ukurasa wake wa Instagrama Daxo chali aliweka wazi hilo kwa kuandika;

Nimeamua Kuacha Kuwasimamia , Juhudi Zangu Zimewafikisha Hapo. So Yeyote Atakayeweza Kuwaendeleza Please Awasaidie. Nitafurahi Nikiona Wanaendelea Nakufanikiwa , 🙏🏽 Ni Wasanii Wazuri Sana Wakipata Mtu Akawapatia KuwaPanga. Mapungufu Yapo Kwa Kila Mtu

Muimbaji Haitham akizungumza na E-Newz ya EATV amesema chanzo cha hayo yote ni katika mtandao wa Instagram ambapo Daxo Chali anamiliki akaunti za wote wawili na kuangalia nini kinaendelea na alipokuta Nini anachati na fulani ambaye inadaiwa kuwa ni boyfriend wake, Daxo  hakuridhika na mazungumzo hayo ndipo alipochukua uamuzi huo.

“Wakati Nini anachati na Boyfriend wake nafikiri Daxo aliona, siwezi kufahamu walikuwa wanachati nini au ulikuwaje lakini tu after hours Nini ananipigia simu ananiambia Kim page yangu imebadilishwa password, so yeye hakumuuliza chochote Daxo” amesema Haitham.

“Baada ya muda akaona kwenye bio zile detail za kumthibitishia yeye ni msanii wa MJ Records zimefutwa, baadaye Daxo ananitumia sms kuwa Nini siyo msanii wangu, nilipoulizwa akiniambia mahusiano ya Nini na Nay wa Mitego yanaharibu CV ya studio, Aseme ni nini anachokita lakini kusema ni mahusiano, no!, kwa sababu kila mtu ana haki ya kupenda” ameongeza.

Daxo Chali

Kwa upande wake Nay amesema jambo hilo halina ukweli wowote na kueleza kuwa jambo hilo haliingi akilini na inadhihirisha upuuzi uliopitiliza

“Sijalipenda kwa sababu nimehusihwa kwenye vitu ambavyo si vya msingi, unamhusisha mtu ambaye atafanya wewe uonekane ni mpuuzi. Nitoe tu ushauri kwa brother Master Jay aangalie MJ Records ni label kubwa kumkabidhi mtoto na kuanza kufanya ujinga, inachafua na inatia doa” amesema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents