Burudani
Wiz Khalifa akamatwa akijisaidia hadharani
Rapper Wiz Khalifa Jumamosi iliyoisha alijikuta matatani baada ya kukamatwa na polisi akijisaidia haja ndogo hadharani.
Tukio hilo lilitokea mida ya saa nane na nusu usiku huko Pittsburgh, Marekani.
Khalifa, ambaye jina lake halisi ni Cameron Jibril Thomaz, alikuwa ametoka kutumbuiza kwenye tamasha la Midnight Madness.
Lil Wayne alitumbuiza pia.