Tupo Nawe

Wiz Khalifa na Amber Rose sasa ni mume na mke baada ya kufunga ndoa kimya kimya!

“I now pronounce you husband and wife….you may kiss the bride”!! Hatimaye couple nyingine ya mastaa (Wiz Khalifa na Amber Rose) imeiaga kambi ya ukapela baada ya kutimiza hitaji muhimu katika mahusiano kwa kufunga pingu za maisha na kubadilisha status za maisha yao sasa kuwa mume na mke.

Wiz n Amba

Jana (July 8) Rapper Wiz Khalifa ametoa taarifa hiyo kwa kutweet “Me and Amber got married today. Weddings this fall. Thought I’d let yall know”, na Amber Rose naye alitweet katika akaunti yake “Yay me & my Baby are officially married!!!”.

Dalili za couple hii kuwa na mpango wa kuhalalisha mahusiano yao kwa kufunga pingu za maisha zilianza kuonekana wiki iliyopita (July 2) baada ya wawili hao kuonekana eneo la kuchukulia leseni ya ndoa japo haikuwekwa wazi ni lini wanampango wa kukamilisha zoezi zima la ndoa.

Rapper wa “Black and Yellow” Wiz Khalifa mwenye miaka 25 alimvisha pete ya uchumba Amber Rose mwenye miaka 29 (march) 2002 na kuufahamisha ulimwengu kwa kutweet “She Said Yes!!!” na kuweka picha ya Amba Rose akiwa na pete ya uchumba katika akaunti yake ya Instagram.

Couple hii ilifanikiwa kupata mtoto wa kwanza wa kiume mwezi (February) mwaka huu waliyempa jina la Sebastian Taylor Thomaz.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW