Wiz Khalifa na mpenzi wake Izabela waachana, yadaiwa Khalifa bado ana mahusiano na Ex wake

Msanii Wiz Khalifa na Izabela Guedes hawako tena pamoja baada ya kufuta wawili hao kufuta picha zote walizopostiana kwenye mitandao ya kijamii na inasemekana kwamba Khalifa amekuwa akitembea na mwanamke mwingine ukiacha na Izabela.
Wiz Khalifa na Izabela Guedes ambao walianza kuwa pamoja mwaka 2016.

Sources ambazo zipo karibu na wawili hao zimewaambia MediaTakeOut.com kwamba Isabela ameachana na Wiz kwa sababu yeye bado anahisi Wiz anatoka na Ex wake wa zamani.

Watu wengi wanashaka kwamba Ex huyo akawa ni Amber Rose.

Rose kwa sasa ni mchumba wa rapa 21 Savage na wapenzi hao wanaenda kila mahali pamoja.

Hapo nyuma Wiz Khalifa alishawahi kuwa na mrembo Indya Marie,Indya Marie pamoja na María Becerra.

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW