Habari

Wizara ya Elimu yatoa agizo Bodi ya Mikopo, wanafunzi wa UDSM

Wizara ya Elimu imeiagiza bodi ya mikopo kukutana na uongozi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (DARUSO) leo Disemba 16 kutatua changamoto zinazokwamisha wanafunzi wa UDSM kupewa mikopo yao.

Agizo hilo limekuja baada ya wanafunzi hao kutoa saa 72 hapo jana kupewa mikopo au wataandamana.

”Wizara imepokea taarifa ya kuwepo changamoto za mikopo ya wanafunzi wa UDSM. Imeiagiza Bodi ya Mikopo na Uongozi wa Chuo kukutana na DARUSO leo kutatua changamoto hizo. Wizara inawataka wanafunzi kuwa watulivu na kuendelea na masomo wakati changamoto hizo zikishughulikiwa.” Imeandika Wizara ya Elimu kupitia akaunti yake ya Twitter.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam wametishia kwenda kukusanyika katika Ofisi ya Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu, (HELSB), endapo ndani ya saa 72 watakuwa hawajawaingizia fedha baadhi ya wanafunzi ambao ni wanufaika wa mkopo.

Maazimio ya wanafunzi wa UDSM dhidi ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu. DARUSO imetoa saa 72, bodi iwe:

i. Imepeleka fedha za wanafunzi chuoni

ii. Imerudisha fedha za wanafunzi zilizokatwa

iii. Imewapangia mikopo waliokata rufaa

iv. Imbadili afisa mikopo chuoni hapo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents