Habari

Wizara yaingilia mgomo wa wanafunzi Azania

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi imetoa tamko la kuitaka shule ya Sekondari ya wavulana ya Azania itafute ufumbuzi wa matatizo ya mgomo unaowasumbua wanafunzi hao.

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi imetoa tamko la kuitaka shule ya Sekondari ya wavulana ya Azania itafute ufumbuzi wa matatizo ya mgomo unaowasumbua wanafunzi hao.


Akizungumza katika kikao cha walimu na wanafunzi hao, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Elimu ya Sekondari, Dickson Ndabise alisema wizara itahakikisha jambo hilo linashughulikiwa mara moja ili kuwaepusha wanafunzi hao kupata madhara.


Alisema suala la maji tayari wizara imeshawasiliana na Mamlaka ya Maji safi Dawasco kuja kurekebisha hali hiyo na kuahidi kuwa suala hilo litashughulikiwa ndani ya siku tatu.


Ujumbe wa wizara hiyo uliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Patrick Tsere ambaye alisema madai ya wanafunzi hao ni ya msingi kujionea hali ilivyo na hasa uchafu wa vyoo uliosababishwa na ukosefu wa maji.


Alisema alikwenda hapo kuhakisha ulinzi na amani unapatikana lakini suala la kutatua matatizo yao yatatatuliwa na wizara kwa sababu wameshatuma wawakilishi wao hapo.


Mapema jana asubuhi wanafunzi hao waliandamana mpaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambapo walishauriwa kurudi shuleni kwa kuwa maafisa wa wizara wameshatumwa kwenda kutataua tatizo lao.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents