Wizi wa mitihani wakithiri Kanda ya Magharibi

KANDA ya Magharibi yenye mikoa ya Tabora, Kigoma na Shinyanga inakabiliwa na tatizo kubwa la udanganyifu wa mitihani ambayo inafanywa.

Na Robert kakwesi,Tabora


KANDA ya Magharibi yenye mikoa ya Tabora, Kigoma na Shinyanga inakabiliwa na tatizo kubwa la udanganyifu wa mitihani ambayo inafanywa.


Kauli hiyo imetolewa na Mkaguzi Mkuu wa Shule Kanda ya Magharibi, Bakari Haruna,alipokuwa akitoa matokeo ya mtihani wa Kitaifa kwa Kidato cha Pili, Kanda ya Magharibi.


Alisema tatizo la udanganyifu katika mitihani limekuwa kubwa, hivyo ni vema jamii ikaelimishwa kuhusu madhara ya udanganyifu katika mitihani ili kuondokana na tatizo hilo.


Haruna alisema kutokana na udanganyifu katika mitihani iliyofanywa ya Kidato cha Pili, jumla ya wanafunzi 213 kutoka shule 41 wamefutiwa matokeo yao katika Kanda ya Magharibi.


Alibainisha kwamba kati ya wanafunzi hao waliofutiwa matokeo yao, Mkoa wa Shinyanga unaongoza kwa kuwa na wanfunzi 110 waliofutiwa matokeo yao,ukifuatiwa na Mkoa wa kigoma wenye wanafunzi 81 na Tabora ina wanafunzi 22 waliofutiwa matokeo.


Mtihani huo umefanywa na wanafunzi 33,155 wakati walijiandikisha walikuwa wanafunzi 36,311 ambapo asilimia 90 wamefaulu katika madaraja mbalimbali huku wanafunzi 3,278 wakishindwa kwa kupata daraja la F.


Matokeo hayo yanaonyesha shule za binafsi na seminari zimetamba katika shule kumi bora kwa kuwa na jumla ya shule tisa,binafsi shule sita na seminari shule tatu huku serikali ikiambulia shule moja tu.


katika shule kumi zilizofanya vibaya tisa ni za wananchi na moja ya binafsi ambapo pamoja na kufanya vibaya,shule za wananchi zimetamba kwa kuingiza wanafunzi watatu waliofanya vizuri katika wanafunzi kumi bora huku msichana pekee,Tumaini Seleman akishika nafasi ya tisa katika wanafunzi hao kumi bora.


Waliofanya mtihani wa kidato cha pili mwaka 2005 katika kanda ya Magharibi walikuwa 21,989 wakati walioandikishwa walikuwa 23,555 na waliofaulu ni asilimia 77 hivyo kufanya ongezeko la wanafunzi 11,166 waliofanya mtihani mwaka 2006,ongezeko linalotokana na kuandikishwa kwa shule nyingi za wananchi.


Source: Mwananchi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents