Burudani

Wizkid aingia kwenye orodha ya mastaa wanaolipwa mkwanja mrefu zaidi kwenye show za mialiko duniani (+video)

Msanii wa muziki kutoka Nigeria,  Wizkid ameingia kwenye orodha ya mastaa wa muziki duniani wanaolipwa mkwanja mrefu zaidi kwa kutumbuiza kwenye show za mialiko maalum.

Wizkid ameingia kwenye orodha hiyo baada ya kutumbuiza kwenye harusi ya kifalme nchini India wikiendi iliyopita, ambapo inaelezwa kuwa alilipwa alilipwa Rupee Milioni 50 (dola $681,200) ambayo ni sawa na Tsh. Bil. 1.6 .

Ukumbi na eneo ambalo Wizkid alienda kutumbuiza linajulikana kama Umaid Bhawan Palace moja ya maeneo yanayoheshimika India na duniani kote.

Image result for umaid bhawan palace

Hata hivyo, mwenyewe baada ya show hiyo alithibitisha kwa ku-tweet kuwa ni kweli amepokea mkwanja mrefu japokuwa hakutaja kiasi.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents