Burudani

Wizkid atambulisha ndinga yake mpya aina ya Lamborghini akiwa Dubai

Wizkid atambulisha ndinga yake mpya aina ya Lamborghini akiwa Dubai

Msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria Ayodeji Ibrahim Balogun kwa jina maarufu Wizkid ambaye amekuwa kwenye kiwango kizuri kabisa cha muziki na kufanikiwa kuwa miongoni mwa wasanii bora kabisa katika bara la Afrika na sasa akiendelea kuupeleka muziki wa kiafrika duniani.

Ikumbukwe kwamba Wizkid alifanikiwa kufanya show ambayo ilivunja rekodi nchini Marekani katika ukumbi wa Skyway theater Minnesota Octoba 6 mwaka huu.

Lakini pia majuzi tarehe 28 mwaka huu Wizkid ameingia kwenye orodha ya mastaa wa muziki duniani wanaolipwa mkwanja mrefu zaidi kwa kutumbuiza kwenye show za mialiko maalum.

Wizkid ameingia kwenye orodha hiyo baada ya kutumbuiza kwenye harusi ya kifalme nchini India wikiendi iliyopita, ambapo inaelezwa kuwa alilipwa alilipwa Rupee Milioni 50 (dola $681,200) ambayo ni sawa na Tsh. Bil. 1.6 .

Ukumbi na eneo ambalo Wizkid alienda kutumbuiza linajulikana kama Umaid Bhawan Palace moja ya maeneo yanayoheshimika India na duniani kote. Hata hivyo, mwenyewe baada ya show hiyo alithibitisha kwa ku-tweet kuwa ni kweli amepokea mkwanja mrefu japokuwa hakutaja kiasi.

Baada ya kufanya show hiyo ya India sasa msanii huyo anaelekea Dudai na tayari ameonekana akila bata Dubai,mbali na kula bata huko pia ameitambulisha ndinga yake mpya aina ya Lamborghini ambayo ameipost kwenye Insta stori yake.

Wizkid ndio msanii pekee kutoka Nigeria aliyewahi kuvunja rekodi ya kufikisha Views milioni moja kwenye nyimbo yake ndani ya masaa 20 kupitia mtandao wa VEVO kwenye nyimbo yake ya “Fever”

By Ally Juma.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents