Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Wizkid atimiza ahadi yake kwa mashabiki

Msanii Wizkid ametimiza ahadi yake leo Jumatatu ya kuachia ngoma yake mpya aliyofanya na mkongwe wa muziki nchini Nigeria, 2Face.

Wiz alitoa taarifa za kuachia wimbo huo uitwao ‘Medicine’ kuanzia Jumapili hii kupitia mtandao wa Twitter. Mkali huyo wa ‘Come Closer’ yupo mbioni kuachia ngoma yake nyingine aliyofanya na mwanadada Tiwa Savage.

Wakati huo huo muimbaji huyo ametajwa kutumia masaa 48 ambayo ni sawa na siku mbili kuandaa albamu yake mpya inayotarajiwa kutoka siku yoyote kuanzia sasa. Usikilize wimbo huo mpya wa Wizkid na 2Face hapa chini.

Na Laila Sued

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW