DStv Inogilee!

Wizkid awapigia magoti mashabiki

Msanii kutoka nchini Nigeria, Wizkid amewapigia magoti mashabiki zake kwa kushindwa kuhudhuria tamasha la muziki la Made in America (MIA)2017.

Tamasha hilo lilifanyika kwa siku mbili mfululizo maeneo ya Philadelphia, kwenye uwanja wa Benjamin Franklin Parkway. Kupitia mtandao wa Twitter, msanii huyo ameomba radhi mashabiki  kwa kosa hilo.

“Apologies to my fans in philly! Missed made in america yesterday but will make it up in a major way! ❤️,” ameandika Wizkid. Pia msanii huyo akawajulisha mashabiki zake kuwa ifikapo tarehe 29 mwezi huu atakuwa na tamasha lingine Uingereza hivyo wasikose.

Tamasha la MIA 2017 limeudhuliwa na muandaaji wa tamasha hilo Jay Z  pamoja na wasanii kama J.Cole, Migos, Solange, Pusha T, Run the Jewels, Vic Mensa, DMX, 21 Savage,Sampha  na Ugly God, Rob Stone, PnB Rock, KYLE, A Boogie Wit Da Hoodie, na wengineo

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW