Burudani

Wizkid aweka wazi muda wa kuachia ngoma aliyofanya na rapper Future

By  | 

Je unatamani kuisikia ngoma mpya ya Wizkid na Future kutoka Marekani? Basi kaa tayari kulina hilo.

Wizkid amethibitisha hilo katika mtandao wake wa Twitter kuwa ifikapo Jumatano majira ya saa tisa mchana kwa saa za Afrika Mashariki ambapo kwa Nigeria itakuwa ni saa saba mchana, wataachia wimbo wao huo mpya.

“Wizkid x Future tomorrow! 1pm naija Time!! ?? ?,” ameandika Wiz kwenye mtandao huo.

Wakati huo huo Julai 22 mwaka huu wakati wa tamasha la Castle Light Unlocks lililofanyika katika viwanja vya Leaders, rapper Future alipoongea na waandishi wa habari alithibitisha kuwa tayari ameshafanya ngoma na Wizkid.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments