Burudani

Wizkid kupitia wimbo wake wa ‘Daddy Yo’ alamba dili nono Uingereza

Msanii wa Muziki kutoka Nigeria, Wizkid kupitia wimbo wake wa ‘Daddy Yo’ ambao aliutoa mwaka jana amefanikiwa kupata dili nono nchini Uingereza, ambapo wimbo huo utatumika kama Soundtrack kwenye filamu ya ‘Pacific Rim Uprising’ iliyoigizwa na John Boyega.

Wizkid

 

Taarifa hizo zimethibitishwa na Muigizaji wa filamu hiyo,  John Boyega ambapo kupitia ukurasa wake wa Twitter ameposti kipande cha video ya wimbo huo huku akicheza na kuandika “Moja ya vitu vinavyonifurahia  kwenye nyuma ya pazia ya utengenezaji wa filamu ya Pacific Rim Uprising ni kuvipa nafasi vipaji kushawishi watu. Ndio maana nimeamua kuweka wimbo wa ‘Daddy Yo’ wa Wizkid kwenye filamu.

Wizkid pia amelipokea dili hilo kwa mikono miwili kwa kumjibu “Thanks My Bro!” kwenye tweet hiyo, Filamu hiyo inatoka mwezi Machi 23 mwaka huu na inasubiriwa kwa hamu na wapenzi wa filamu duniani kote.

Tazama Trailler ya Movie hiyo hapa chini;

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents