BurudaniUncategorized

Wizkid kutumbuiza Wasafi Festival Dar Es Salaam

Wizkid kutumbuiza Wasafi Festival Dar Es Salaam

Msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria Ayodeji Ibrahim Balogun maarufu,  Wizkid anatarajiwa kutumbuiza katika tamasha la Wasafi Festival litakayofanyika Dar Es Salaam baada ya Diamond kuthibitisha hilo.

Rais huyo wa WCB amethibitisha hilo kupitia ukurasa wa Instagram baada ya ku-comment kwenye post ya Rayvanny ambayo alipost video fupi ikiwaoyesha Diamond na Wizkid muda mfupi baada ya kumalizika kwa tamasha kubwa la muziki la One African Music Festival lililofanyika Dubai wikiendi iliyopita.

Kupitia video hiyo hapo juu Wizkid  alisikika akisema muda sio mrefu wimbo wao na Diamond utatoka na ndipo Diamond alipothibitisha kuwa mwimbaji huyo atatua kwenye tamasha hilo litakalofanyika Dar Es Salaam baada ya kuzunguka mikoa mingine.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents